SIMBA SC YAMTAMBULISHA KIUNGO MAEMA

Nyota mpya Simba SC, raia wa Afrika Kusini Neo Maema ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi hicho Agosti 21 2025 kuelekea msimu mpya wa 2025/26.

Huyu ni kiungo mshambuliaji ambaye yupo na timu kambini nchini Misri alikuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini, maarufu kwa jina la Bafanabafana kwenye CHAN 2024.

Nyota huyo alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Mamelodi Sundowns alidumu hapo kwa misimu minne akiwa kwenye majukumu yake ya kazi.

Simba SC kwa sasa inaendelea na maandalizi chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ambaye ni raia wa Afrika Kusini.

Inatarajiwa kurejea Tanzania hivi karibuni kwa maandalizi ya mwisho kuelekea msimu mpya ambapo Septemba 10 2025 ni siku maalumu ya Simba Day kutambulisha uzi mpya, wachezaji na benchi la ufundi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.