MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wameanza kukusanya makombe kuelekea msimu mpya wa 2025/26 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Amahoro.
Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Aziz Andambwile wa Yanga SC ambaye alijifunga dakika ya 2, bao hilo lilisawazishwa na Boyel mshambuliaji mpya wa Yanga SC, bao la pili lilifungwa na Pacome dakika ya 45.
Wakati mpira ukiwa unakaribia kufika ukingoni, nahodha wa Yanga SC, Bakari Mwamnyeto alifunga bao la tatu dakika ya 90+4 na Yanga SC ikatwaa taji la Rayon Sports Cup.
Huu ni mchezo wa kwanza wa ushindani kwa Yanga SC kuelekea msimu wa 2025/26 chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz ambapo ball ilitembea.
Mabao yote manne kwenye mchezo huo yalifungwa na Yanga SC wenyewe huku wenyeji wakikwama kufunga kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.