Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamempitisha kwa kishindo Rais wa sasa, Wallace Karia, baada ya kumpigia kura za ndiyo kwa asilimia 100.
Karia alikuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais, kufuatia wagombea wengine kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi kwa kushindwa kutimiza vigezo vya kikanuni.
Kwa ushindi huo, Karia anaendelea kuiongoza TFF katika muhula mpya, huku wajumbe wakionesha imani kubwa kwake katika kuendeleza maendeleo ya soka la Tanzania.
WALLACE KARIA APITISHWA TENA KUONGOZA TFF KWA ASILIMIA 100
