RASMI Azam FC imewatambulisha wachezaji wapya wawili ambao watakuwa chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ipo wazi kwamba Azam FC itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ambapo itaanzia hatua za awali na mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa ugenini katika kusaka ushindi.
Ni Baraket Ihmid ambaye ni winga kutoka Tunisia Taieb Ben Zitoun huyu ni mshambuliaji alikuwa anacheza Al Hilal hivyo msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya Azam FC.
Wachezaji hao wamesaini kandarasi ya miaka miwili watakuwa hapo mpaka 2027. Ikumbukwe kwamba Agosti 12 2025 Azam FC ilimtambulisha Edward Manyama ambaye ni beki kwa kadarasi yam waka mmoja imeweka kambi nchini Rwanda.
Kwenye anga la kimataifa Azam FC imepangwa kucheza dhidi ya Al Merriekh Bentui ya Sudan Kusini, kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC 1st Preliminary Round).
Kampeni ya michuano hiyo, itaanzia ugenini kati ya Septemba 19-21, mchezo wa pili Azam FC itakuwa nyumbani Uwanja wa Azam Complex kati ya Septemba 26-28, mwaka huu.
Ikiwa Azam FC itapenya hatua hiyo, itakutana na mshindi wa jumla wa mechi nyingine kati ya AS Port ya Djibout dhidi ya KMKM ya Zanzibar, kabla ya kutinga hatua ya makundi. Droo hiyo ilichezwa Agosti 9 katika studio za Azam TV, Dar.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.