Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli (24) kama mchezaji mpya wa kikosi hicho kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja kutoka Sekhukhune United ya Afrika Kusini, ukiwa na kipengele cha kununuliwa kabisa mwishoni mwa mkataba.
Boyeli anasifika kwa uwezo mkubwa wa kufumania nyavu na alijizolea umaarufu mkubwa msimu wa 2022/23 akiwa na Power Dynamos ya Zambia, ambapo:
Alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP)
Alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Zambia kwa mabao 18
Ujio wake unaongeza nguvu mpya kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga SC inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.