PACOME ZOUZOUA KUBAKI YANGA MPAKA 2027

Kiungo mahiri kutoka Ivory Coast, Pacome Zouzoua,inasemekana ameshasaini mkataba mpya na klabu ya Yanga SC siku nyingi zilizopita, muda mfupi tu baada ya fainali ya Kombe la CRDB.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, mkataba huo wa miaka miwili ulitayarishwa na kusainiwa kipindi hicho, huku mpunga ukishalipwa rasmi fedha ambazo Zouzoua hakupoteza muda kuzitumia kujenga jumba la kifahari kwao Ivory Coast.

Kwa sasa, kinachosubiriwa ni kurejea kwake Bongo, muda wowote kuanzia sasa, ili aungane na timu katika maandalizi ya msimu mpya (Pre-season).

Kumbuka, msimu wa 2024/25 ulikuwa wa kifalme kwa Zouzoua, baada ya kutwaa tuzo ya MVP kutokana na kutikisa ligi kwa tuzo nyingi za Mchezaji Bora wa Mechi katika mizunguko mbalimbali.

Yote yamewekwa wazi Pacome Zouzoua atasalia kuitumikia Yanga SC hadi mwaka 2027. Mashabiki wa Wananchi, mna sababu ya kutabasamu!