KITABU CHA MOYO WANGU UNAVUJA DAMU RASMI KIPO MTAANI

LEO Julai 24, 2025, kitabu kipya kiitwacho Moyo Wangu Unavuja Damu kimetambulishwa rasmi sokoni katika Makao Makuu ya Global Group, Sinza – Mori, ikiwa ni kazi ya pili ya fasihi kutoka kwa mtunzi mahiri Lunyamadzo Mlyuka, aliyejipatia umaarufu kupitia kitabu chake cha awali Ganzi ya Maumivu.

Kitabu hiki ni simulizi ya kusisimua inayochambua kwa kina jitihada za vijana katika kuyafikia malengo yao, pamoja na changamoto zilizojificha ndani ya familia za Kiafrika katika malezi na maisha ya kila siku.
Tunakutana na mhusika mkuu, Christopher, kijana kutoka familia ya kipato cha chini, ambaye licha ya kuwa na ndoto kubwa, anakumbana na vizingiti vya maisha vinavyotishia mustakabali wake.

Mbali na simulizi hiyo ya kuamsha fikra, kuna zawadi ya kipekee ya kitabu cha Tabasamu kilichomo ndani ya Moyo Wangu Unavuja Damu  zawadi hii ni kwa ajili yako msomaji mpenzi. Usikubali kuikosa! Kitabu kimeshawasili mtaani, kinapatikana sasa.

Pata nakala yako (Soft Copy au Hard Copy) kupitia:
📞 +255 756 028 371
📧 thisisdizo444@gmail.com