VICTOR GYÖKERES KUJIUNGA NA ARSENAL

Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano na Sporting Lisbon kuhusu usajili wa mshambuliaji raia wa Sweden, Victor Gyökeres, kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia €63.5 milioni pamoja na nyongeza ya hadi €10 milioni kulingana na mafanikio mbalimbali.

Gyökeres (27) anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utamweka Emirates hadi Juni 2030.

Mshambuliaji huyo aliyeng’ara msimu uliopita kwa mabao na pasi za mabao, anatajwa kuwa chaguo muhimu kwa kocha Mikel Arteta katika kuimarisha safu ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya England.