YANGA SC YAMALIZANA NA BEKI WA KAZI

INAELEZWA kuwa Yanga SC mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25 likiwa ni taji lao la 31 wamekamilisha usajili wa staa wa kimataifa wa Guinea, Balla Moussa Conte

Conte ni staa wa kimataifa wa Guinea ambaye anakipiga kwenye Klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia. Taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Bongo kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo huyo, kabla ya Simba SC kumpandia dau baada ya maelekezo ya kocha wao mkuu, Fadlu Davis.

Hivyo kuna makubaliano ambayo yamefanyika kati ya CS Sfaxien na Yanga, ambapo Yanga walipewa ruhusa ya kuzungumza na mchezaji Conte, kabla makubaliano ya mchezaji na Yanga SC ilielezwa kuwa Simba SC walimfuata na ofa kubwa.

Simba SC iliwafuata CS Sfaxien baada ya mchezaji huyo kupitishwa jina lake na kocha Mkuu Fadlu ambapo taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC wamekamilisha dili la kumpata nyota huyo kwa asilimia kubwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.