SIMBA SC iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC 2024/25 bado ipo kwenye mchakato wa kuendelea kujenga kikosi.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 ndani ya ligi namba nne kwa ubora bingwa ni Yanga SC akitwaa taji la 31 chini ya kocha Miloud Hamdi ambaye hatakuwa katika kikosi hicho kwa msimu wa 2025/25.
Kwa mujibu wa Rais wa Heshima wa Simba SC, Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo amebainisha kuwa msimu uliopita haukuwa mwepesi ulikuwa na changamoto nyingi lakini wanaendelea kuimarika taratibu.
“Msimu uliopita haukuwa mzuri kwetu na haukuwa rahisi. Tumepitia mengi na tunaamini kwamba bado tunajipanga upya kwa msimu ujao.
“Sisi bado tupo kwenye mchakato wa kujenga kikosi upya ambapo tulianza kazi hiyo msimu ambao umekwisha bado hatujafanikiwa kufikia malengo yetu hivyo tunaendelea kujenga kikosi upya.
“Tumefanikiwa kupelekea timu kwenye fainali ya Afrika mara mbili licha ya kwamba hizo zote tulishindwa kupata ushindi hii inaonyesha bado tunazidi kupanda. Timu yetu ipo nafasi ya tano Afrika na malengo makubwa ni kuona kwamba tunaleta ubingwa wa Afrika.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.