MATOKEO YA KIDATO CHA SITA NA UALIMU MEI 2025, YAPO HAPA

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) pamoja na Mitihani ya Ualimu iliyofanyika mwezi Mei 2025.

Matokeo hayo yanapatikana kupitia tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz), ambapo wanafunzi na walimu waliohusika wanaweza kuyatazama kwa kutumia namba za mtihani au majina ya shule na vituo husika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mtendaji wa NECTA, matokeo hayo yanaonesha kuongezeka kwa ufaulu ikilinganishwa na mwaka jana, huku shule kadhaa zikiongoza kwa viwango vya juu vya matokeo ya daraja la kwanza na la pili.

Aidha, matokeo ya Mitihani ya Ualimu kwa ngazi ya Diploma ya Ualimu wa Sekondari na Msingi pia yametolewa, yakionesha hali ya kuridhisha ya watahiniwa wengi katika masomo ya msingi ya kitaaluma.

NECTA imesisitiza kuwa wanafunzi waliopata changamoto ya kuona matokeo yao wanatakiwa kuwasiliana na uongozi wa shule au kufuatilia taarifa zaidi kupitia ofisi za mikoa au tovuti ya baraza. BONYEZA HAPA CHINI

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU (DSEE) 2025

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU (GATCE) 2025

MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU (GATSCCE) 2025