AZIZ KI WA YANGA SC KUCHEZA HAPA BONGO

MFUNGAJI bora ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika, Aziz Ki msimu wa 2023/24 huenda akarejea kwa mara nyingine ndani ya ardhi ya Tanzania.

Ki alifunga jumla ya mabao 21 alipokuwa namba moja. Timu ya Yanga SC ilitwaa ubingwa wa ligi na Azam FC ilikuwa nafasi ya pili.

Mei 24 2025 Ki alitoa Thank You kwa mabosi wake Yanga SC baada ya kupata changamoto mpya nchini Morocco. Taarifa zinaeleza kuwa huenda akarejea Yanga SC kwa msimu wa 2025/26.

Kiungo huyo alipata dili la kujiunga na Wydad Casablanca ya Morocco. Benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Mohammed Amin Benhashem wa Wydad linatajwa kutoridhishwa na kiwango chake.

 Ally Kamwe Ofisa Habari wa Yanga SC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC 2024/25 amefungukia suala la Ki kurudi ndani ya timu hiyo. Kamwe alibainisha kuwa kila kitu kipo kwenye makubaliaono. Alieleza kuwa Ki mkataba wake ulikuwa na vipengele muhimu.

“Kwa mujibu wa makubaliano ilikuwa hadi kufikia Julai 10 Wydad wawe wameshawasiliana na Yanga SC. Kama Wydad watakuwa wanaongeza maana yake wamalizie kiasi ambacho tulikubaliana ila kama watasema arudi sawa arudi aje awashone. Bado amebaki na mwaka mmoja,” amesema Kamwe.

Msimu wa 2024/25 mchezo wake wa mwisho kabla hajasepa Bongo Aziz Ki ulikuwa wa CRDB Federation Cup dhidi ya JKT Tanzania. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.