ENG. HERSI SAID AENDELEA KUIBEBA SOKA LA AFRIKA KUPITIA ACA

Mwaka uliopita, Chama cha Umoja wa Vilabu Afrika (ACA) chini ya uongozi wa Eng. Hersi Said, kilifanikiwa kushawishi CAF kutoa dola 50,000 kwa kila klabu iliyoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho (CAF CC) katika hatua ya awali.

Kwa msimu huu mpya, ACA imeendelea kupigania maslahi ya vilabu barani Afrika kwa mafanikio zaidi. Kupitia mazungumzo na ushawishi wao kwa CAF, imeidhinishwa kuwa klabu zitakazoshiriki hatua ya awali ya CAF CL na CAF CC zitalipwa dola 100,000 kila moja kwa ajili ya maandalizi.

Ikumbukwe, kabla ya uwepo wa ACA, klabu shiriki katika hatua za awali za mashindano hayo hazikuwa zikipewa msaada wowote wa kifedha na CAF.

Hatua hii imepongezwa na wadau wengi wa soka barani Afrika kama ishara ya kweli ya mapambano ya kuleta usawa na maendeleo ya vilabu vya Afrika vilivyo katika mazingira magumu ya kifedha.

Kwa mara nyingine tena, Eng. Hersi Said ameendelea kuthibitisha kujitolea kwake kwa dhati katika kuendeleza soka la Afrika na kupigania maslahi ya vilabu.

“Hersi anazidi kuipambania football ya Afrika.” – @alikamwe