Baba mzazi wa mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, Mzee Ally Samatta, amefariki dunia asubuhi ya leo, Julai 6, 2025.
Msiba upo Mbagala, jijini Dar es Salaam, ambapo familia, ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika kuomboleza msiba huo mzito.
Timu ya Global TV ipo eneo la tukio na itaendelea kukuletea taarifa kamili kuhusu msiba huu, ikiwemo ratiba ya mazishi, ujumbe wa familia, na yale yote yanayoendelea nyumbani kwao Samatta.
Taarifa zaidi zitafuata. Pole kwa familia ya Samatta, wapendwa na mashabiki wote wa soka nchini.