MIGUEL GAMONDI ATANGAZWA KOCHA MPYA WA SINGIDA BLACK STARS

Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha rasmi kumteua Miguel Ángel Gamondi kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja, kuelekea msimu wa mashindano wa 2025/2026.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo, imeelezwa kuwa uamuzi huo ni sehemu ya mpango wa kuimarisha kikosi na kuongeza ushindani katika ligi kuu na michuano mingine. Taarifa hiyo ilisomeka:

“Bodi ya Wakurugenzi ya Singida Black Stars imefanya mabadiliko ya kiufundi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya. Lengo ni kuhakikisha timu inakuwa imara zaidi na inashindana kwa mafanikio.”

 Benchi la Ufundi Lapanuliwa:

Sambamba na ujio wa Gamondi, klabu hiyo pia imetangaza kuwa David Ouma (raia wa Kenya) na Moussa N’Daw (raia wa Senegal) watakuwa Makocha Wasaidizi, wakishirikiana kwa karibu kuhakikisha timu inapata matokeo bora.