LIVERPOOL WATOA TAARIFA KUHUSU DIOGO JOTA

NYOTA Diogo Jota, ametangulia mbele za haki kwa ajali akiwa na miaka 28 tu. Mchezaji huyo wa mpira wa lipoteza maisha yake katika ajali ya gari iliyotokea Zamora karibu na mpaka wa Kaskazini-Magharibi kati Uhispania na Ureno. Katika gari hiyo alikuwa na kaka yake ambaye naye ametangulia mbele za haki.

 Waajiri wake Liverpool mabingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2024/25 wametoa taarifa kuhusu Jota. Mapema Liverpool inayoshiriki Premier League ilikuwa haijatoa taarifa baada ya tukio kutokea.

“Klabu ya Soka ya Liverpool imesikitishwa na kifo cha Diogo Jota. Klabu imearifiwa kwamba Jota mwenye umri wa miaka 28 amefariki kutokana na ajali ya barabarani nchini Hispania pamoja na kaka yake, Andre.

“Liverpool haitatoa maelezo zaidi kwa wakati huu na inaomba kuheshimiwa kwa faragha ya familia ya Diogo na Andre, marafiki, wachezaji wenzake na wafanyakazi wa klabu wakati wanapojaribu kukabiliana na hasara isiyoweza kufikiriwa. Tutaendelea kuwapa msaada wetu kamili.”

Jota alianza kazi yake na Pacos de Ferreira kabla ya kuhamia Atletico Madrid, Porto na Wolverhampton Wanderers. Alitumia miaka mitatu na Wolves kabla ya kuhamia Liverpool mwaka 2020. Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji waliotwaa taji la ligi ya Premier League.

Rekodi zinaonyesha kuwa Jota alikuwa amecheza mechi 182. Katupia jumla ya mabao 65. Nduguyo Jota, Andre Felipe, pia alifariki katika ajali hiyo, ambayo iliyotokea mapema.

Source: Mirror

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.