YANGA SC YAPOKELEWA KWA KISHINDO, YAWEKA NGOME MSIMBAZI

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara 31, Yanga SC Juni 30 2025 wamepokelewa kwa kishindo wakitokea Zanzibar kwa kufanya pared la kihistoria chini ya uangalizi mkali wa Jeshi la Polisi Tanzania ambao walikuwa wakihakikisha usalama unakuwa wakutosha.

Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, Juni 29 2025 ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars na kutwaa taji la CRDB Federation Cup.

Taji hilo linakuwa ni la tano kwa msimu wa 2024/25 ikiwa ni rekodi kubwa kuandikwa. Walianza na Toyota Cup wakiwa nchini Afrika Kusini, Ngao ya Jamii, Muungano, Ligi Kuu Bara ya NBC na wakafunga kete ya tano na CRDB Federation Cup ambapo hapo walikuwa ni mabingwa watetezi.

Wametetea pia taji la ligi chini Miloud ikiwa ni timu namba moja kufunga mabao mengi ambayo ni 83 na pointi zake ni 82 kibindoni.

Kwenye msafara huo ambao ulianzia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ulipita kwenye vituo kadhaa ikiwa ni Karume, Ilala na Kariakoo huku ukiweka kambi kwa muda yalipo makao makuu ya Simba SC, Msimbazi, Kariakoo.

Hapo mashabiki wa Yanga SC, viongozi wakiongozwa na Rais wa Yanga SC, Injnia Hersi Said walikuwa wakicheza na kufurahi.Wimbo wao chaguo namba moja ilikuwa ni ule wa Ali Kiba, ‘Unyama ni Mwingi’.

Burudani haikuishia hapo walitinga timu makao makuu ya Yanga SC ambapo hapo kulikuwa na burudani kutoka kwa Mbosso na wimbo pendwa ni ule wa Afiola, Makabila ambapo kila mmoja alitoa burudani kwa Wananchi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.