SIMBA SC haijawa na bahati mbele ya Yanga SC kwenye mechi za Kariakoo Dabi. Msimu wa 2024/25 haujawa bora kwao wakifungwa nje ndani ya mtani katika mechi za ligi.
Rekodi zinaonyesha kuwa katika mechi ambazo wamekutana mkali wakucheka na nyavu ni Aziz Ki kwenye misimu mitano ya hivi karibuni kuanzia 2020/21. Ki kafunga jumla ya mabao matatu na kwa sasa hayupo ndani ya kikosi cha Yanga SC akiwa Wydad Casablanca kwenye changamoto mpya.
Juni 25 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC. Pointi tatu zilikuwa mali ya Yanga SC ambayo imetwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya nne mfululizo mbele ya Simba SC.
Kibu Dennis ndiye nyota anayeongoza kufunga mabao mengi kwa Simba SC katika Kariakoo Dabi akiwa na mabao mawili pekee, Simba SC haijawa na bahati kushinda mbele ya Yanga SC, mechi 10, ushindi mchezo mmoja, sare nne na kupoteza 5.
Ndani ya ligi msimu wa 2024/25, Kibu Dennis amefunga jumla ya mabao manne kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC. Kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi alianza benchi na aliingia kipindi cha pili, Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.