YANGA SC WALIPANIA KUIFUNGA SIMBA SC

Dickson Job nahodha msaidizi wa Yanga SC amesema kuwa walikuwa wanahitaji kuifunga Simba SC kwa namna yoyote ile ili kutwaa ubingwa wa msimu wa 2024/25 jambo ambalo lilifanikiwa Juni 25 2025 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

Simba SC ndani ya msimu wa 2024/25 imepishana na mataji yote iliyokuwa inapambania. Taji la CRDB Federation Cup imegotea hatua ya nusu fainali ikindolewa na Singida Black Stars. Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika imegotea nafasi ya pili ikipoteza mbele ya RS Berkane kwenye mchezo wa fainali. Katika ligi ni Yanga SC wametwa ubingwa wakigotea nafasi ya pili.

Mabao kwenye mchezo wa Juni 25 2025 yalifungwa na Pacome ambaye anafikisha mabao 12 ndani ya ligi na Clement Mzize ambaye anafikisha jumla ya mabao 14 akiwa ni mzawa mwenye mabao mengi kwenye ligi msimu wa 2024/25.

Kwenye mchezo namba 184, dakika 45 za mwanzo wababe hao walitoshana nguvu, kipindi cha pili baada ya Clement Mzize kuingia kasi ya ushambuliaji kwa Yanga SC iliongezeka na mwisho ubao ukasoma Yanga SC 2-0 Simba SC.

Job amesema: “Tulikuwa tunatambua kwamba tukipata sare tutakuwa mabingwa wa ligi.Ila sisi hilo tulikuwa hatuhitaji malengo yetu ilikuwa ni kupata ushindi mbele ya Simba SC jambo ambalo limetimia.”

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.