Mshambuliaji wa Yanga SC Clement Mzize amekamilisha msimu wa 2024/24 akiwa na kicheko kutokana na timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi mbele ya Simba SC kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Juni 25 2025 Uwanja wa Mkapa.
Kwenye mchezo huo namba 184 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC. Mabao ya Pacome na Mzize yalitosha kupeleka kilio Unyamani na kicheko Jangwani.
Clement Mzize kafunga jumla ya mabao 14 ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu upande wa wazawa. Mzize ambaye ni chaguo la kwanza la Miloud kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Mzize alikuwa na siku nzuri kazini kwenye mchezo dhidi ya Simba SC. Katika mchezo huo aliingia dakika ya 45 akichukuwa nafasi ya Prince Dube. Alipachika bao dakika ya 87 akitumia pasi ya Pacome na kufikisha mabao 14 kwenye ligi.
Yanga SC ikiwa imefunga mabao 83, kafunga mabao 14 na kutoa pasi tano za mabao. Mechi tatu mfululizo alikuwa kwenye ubora dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji alitoa pasi za mabao kwa Clatous Chama. Kwenye Kariakoo Dabi yeye alifunga bao moja, Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.