YANGA SC 2-0 SIMBA SC, BINGWA MBELE YA MNYAMA

KARIAKOO Dabi dakika 90 zimekamilika kwa ubao kusoma Yanga SC 2-0 Simba SC. Ubingwa ukiwa mali ya Yanga SC. Clement Mzize ambaye alianzia benchi kwenye mchezo wa leo amefanya kazi kubwa kipindi cha pili alipoingia kuchukua nafasi ya Prince Dube.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Pacome dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati na Clement Mzize dakika ya 87 akitumia pasi ya Pacome.

Yanga SC imetetea ubingwa wa ligi mbele ya Simba SC. Pointi zao kibindoni ni 82 huku Simba SC nafasi ya pili na pointi 78.

Mchezaji Pacome wa Yanga SC amefikisha mabao 12 ndani ya ligi msimu wa 2024/25 huku Mzize akifikisha mabao 14. Kinara ni Jean Ahoua mwenye mabao 16 na pasi 9 za mabao yeye ni kiungo mshambuliaji wa Simba SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.