TAARIFA kutoka Simba SC kuwashukuru mashabiki wake kwa ushirikiano ndani ya msimu wa 2024/25 imeshtua huku wakikaa kimya kuzungumzia mchezo wao wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC.
Simba SC ina kibarua cha kucheza mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa Mkapa. Juni 24 2025, Simba SC hawakutokea kwenye mkutano wa mwisho wa maandalizi ambapo Yanga SC walizungumza.
Mapema Simba SC waliandika ujumbe huu kwenye ukurasa wa Instagram: “Kwa Wanasimba wote, asanteni kwa ushirikiano ambao mmetupatia kwa msimu wa 2024/25. Tunajivunia kuwa na mashabiki kama nyie .”
Simba SC imecheza mechi 29 ina mchezo mmoja wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC unaotarajiwa kuchezwa leo Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.
Juni 24 2025, benchi la ufundi la Simba SC ikiwa ni kocha na nahodha hawakutokea kwenye mkutano wa mwisho wa maandalizi kuelekea mchezo huo na walipotafutwa hawakupatikana.
Ahmed Ally , Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Juni 22 2025 alisema kuwa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ulikuwa ni wa mwisho kwa msimu wa 2024/25 wakiwa nyumbani.Kuhusu Juni 25 watatoa taarifa.
“Kiu kubwa ya mashabiki wa Simba SC ni kuhusu tarehe 25. Nichukue fursa hii kuwaambia mashabiki wote wa Simba SC kuwa kama kuna lolote la kuwaambia kuhusiana na tarehe 25, tutawaambia.”
Mchezo wa leo Juni 25 2025, bingwa wa ligi atakabidhiwa zawadi ya kombe la NBC Premier League msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.