YANGA SC vs Simba SC mechi namba 184 inatarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Juni 25 2025 ikiwa ni mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukutana ndani ya uwanja katika dakika 180.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba SC 0-1 Yanga SC. Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 78 inakutana na Yanga SC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 79 kwenye msimamo.
Mshindi wa mchezo wa leo ana uhakika wa kutwaa taji la ligi kwa kuwa kutakuwa na matukio makubwa mawili. Kariakoo Dabi na zawadi ya ubingwa msimu wa 2024/25.
Simba SC awali walikuwa wanatajwa kugomea mchezo huo na hawakutaka kubainisha jambo lolote, waligomea mazoezi Uwanja wa Mkapa na wakagomea mkutano wa maandalizi ya mwisho dhidi ya Yanga SC.
Taarifa rasmi kutoka Simba SC imeeleza kuwa watakuwepo kwenye mchezo namba 184 Uwanja wa Mkapa. “Tutakuwepo” ilieleza taarifa ya Simba SC.
Yanga SC ana faida kwa kuwa yeye anachohitaji ni pointi moja pekee kutangazwa kuwa bingwa wa ligi na Simba SC ili atibue rekodi hiyo chaguo lake ni moja kuvuna pointi tatu mazima.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.