MILOUD Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC wanatambua ugumu wa mchezo huo ambao hauhitaji maneno zaidi ya utendaji kwa wachezaji kutafuta ushindi.
Ni mchezo wa mzunguko wa pili msimu wa 2024/25. Katika ule mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 0-1 Yanga SC na pointi tatu zilikuwa mali ya Yanga SC ambao ni vinara wa ligi.
Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 79 wanatarajiwa kukutana na Simba SC, Juni 25 2025. Simba SC ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 78 zote zimecheza mechi 29.
Miloud amesema kuwa kwenye kila mchezo ambao wanaingia uwanjani mpango mkubwa ni kupata pointi tatu. Mchezo wao wa nne ni fainali kwao kwa kuwa wanahitaji ubingwa.
“Mchezo wa Derby sio mchezo wa kuongea sana, ni mchezo kwa ajili ya wachezaji. Wachezaji wangu wanajua nini haswa tunahitaji kwenye mchezo huo. Tunawaheshimu sana Simba lakini sisi ni Yanga SC tutafanya kila liwezekanalo tuwe mabingwa.
“Tupo tayari kwa mchezo na maandalizi yapo vizuri kikubwa ni utayari na mashabiki wajitokeze kwa wingi. Tumekuwa na mwendo mzuri na wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya kupambania kupata matokeo mazuri.”
Kwenye mchezo uliopita Yanga SC raundi ya 30 ilifunga kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji na Simba SC ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.