TFF YATANGAZA ORODHA YA AWALI YA WAGOMBEA URAIS NA KAMATI YA UTENDAJI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa orodha ya awali ya waliochukua na kurudisha fomu kuomba uongozi katika Shirikisho hilo kwa nafasi za Urais na nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Waliorudisha fomu hizo ni Ally Mayay Tembele, Ally Thabit Mbingo, Mbette Mshindo Msolla, Mustapha Salumu Himba, Shija Richard Shija na Wallace John Karia ambao wanawania nafasi ya Urais.

Waliorudisha fomu za nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Ally Msigwa, CPA Hosseah Lugano, Cyprian Kuyava, Dkt. David Cleopa Msuya, Dkt. Yono Kevela, Evance Mgeusa na Issa Bukuku.

Wengine ni James Mhagama, Juvenalius Rugambwa, Khalid Mohamed, Lameck Nyambaya, Maanya Maanya, Martin Sekisasa, Mohamed Aden, Robert Kajuba, Rocky Mgeju, Saleh Abdullah, Salum Kulunge na Vedastus Lufano.