JUNI 25 2025 sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara zinatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC kutamatika.
Kwa mujibu wa Karim Boimanda, Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) ameweka wazi kuwa mara baada ya mchezo huo kutamatika kutakuwa na sherehe za kukabidhi kikombe cha ubingwa.
“Tumekuwa na msimu mzuri na wenye ushindani mkubwa jambo ambalo limeongeza ushindani na mchezo wa Kariakoo Dabi ni mkubwa na unawavutia watu kutoka ndani na nje ya nchi.
“Unaona tumemaliza mpaka mzunguko wa 30 kwa timu zote kucheza tukisaliwa na mchezo mmoja ambao uliahirishwa. Lakini mbali na mchezo huo wa ligi ambao ni mchezo mmoja ambao umesalia baada ya kutamatika kwa mchezo huo kutakuwa na sherehe za kukabidhi kikombe cha ubingwa.
“Mabingwa wa NBC 2024/25, tulikuwa na msimu mzuri ambao hauhitaji kujielezea kutokana na mechi zote kuchezwa na bado hakuna bingwa. Wanakutana wakiwa na tofauti ya pointi moja.
“Sasa tuna matukio makubwa mawili ambayo yanakwenda kutengeneza kitu kikubwa ndani ya siku moja, mchezo wa Kariakoo Dabi wenyewe ambao ni mkubwa na kitendo cha kukabidhi kikombe cha ubingwa.” Amesema Boimanda.
Waamuzi katika mchezo wa Kariakoo Dabi ni kutoka mataifa matatu, Tanzania, Misri na Somalia. Hivyo asilimia 90 wanatoka nje ya Tanzania.
Mwamuzi wa kati ni Amin Mohamed Amin Omar kutoka Misri, match Commissioner ni Salim Omary Singano kutoka Tanga na Referees Assessor ni Alli Mohamed kutoka Somalia.
Kwenye msimamo Yanga SC ni nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 79 inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 78 zote zimecheza mechi 29.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.