MASTAA HAWA WALIVAA KITAMBAA CHA UNAHODHA MCHEZO MMOJA

KWENYE mchezo wa mwisho kwa Simba SC msimu wa 2024/25 wakiwa Uwanja wa nyumbani, KMC Complex, Juni 22 2025 kitambaa cha unahodha kilitembea katika mikono ya kutosha wachezaji wakibadilishana kutokana na sababu mbalimbali.

Ikumbukwe kwamba ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids nahodha mkuu ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye ni chaguo la kwanza la kocha.

Mbele ya Kagera Sugar, Zimbwe Jr alianzia benchi ni Fabrice Ngoma alikuwa amevaa kitambaa cha unahodha katika dakika za mwanzo za mchezo huo.

Ngoma hakukomba dakika zote 90 aligotea dakika ya 58 nafasi yake ilichukuliwa na Kibu Dennis, wakati anatoka Ngoma alimkabidhi kitambaa beki Che Malone.

Che Malone dakika ya 77 alikitoa na kumkabidhi Shomari Kapombe ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Ladack Chasambi aliyepata maumivu kwenye mchezo huo.

Kapombe alimkabidhi Zimbwe Jr ambaye aliingia dakika ya 82 ya mchezo akichukua nafasi ya Chamou na kufanya mikono minne kuongoza timu hiyo ndani ya mchezo mmoja.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar. Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 78 inatarajiwa kumenyana na Yanga SC Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.