AMIN OMAR KUTOKA MISRI KUCHEZESHA DABI YA YANGA NA SIMBA KESHO

Waamuzi wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba wametangazwa rasmi, ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar kutoka nchini Misri.

Amin Omar ni mwamuzi mwenye uzoefu mkubwa wa kimataifa, aliyechezesha mechi kadhaa za CAF Champions League na kufahamika kwa uthabiti wake katika kusimamia michezo mikubwa.