YANGA SC KUCHUKUA UBINGWA MBELE YA SIMBA SC, WAMSHTUKIA MTANI

UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kuwa pointi zao mbele ya Simba SC zitawapa ubingwa msimu wa 2024/25 katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora.

Yanga SC inaongoza ligi ikiwa na pointi 79 kibindoni baada ya kucheza mechi 29 sawa na Simba SC ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 78.

Ni msimu ambao umekuwa na ushindani mkubwa huku bingwa akienda kupatikana kwenye mchezo wa mwisho kwa wababe hawa kusaka pointi tatu.

Yaga SC ana machaguo mawili ili kupata taji la ligi kushinda ama kuambulia pointi moja katika mchezo huo. Simba SC chaguo lake ni moja kushinda ili kutwaa ubingwa huo.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa wamebakiza mchezo mmoja ambao ni muhimu Juni 25 dhidi ya watani zao wa jadi.

“Wanayanga tumekamilisha mzunguko wa 29 kwa ushindi mkubwa wa mabao 5-0 ila ambacho tulikuwa tunahitaji ni pointi tatu muhimu ili kutwaa ubingwa. Huu ujanja ambao wenzetu wanao sisi tulishalala huko kitambo hivyo tuendelee kuwa pamoja na tujitokeze kwa wingi wa Uwanja wa Mkapa.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.