TAARIFA ZA UJANJA UJANJA KUMONDOA RAIS WALLACE KARIA ZIACHWE

Tayari kuna taarifa kadhaa kutoka katika vyombo mbalimbali nje ya Tanzania kwamba kuna UJANJA unafanywa kwa ajili ya kumuondoa madarakani Wallace Karia.

Inaelezwa eti Serikali ndio imeamua. Wajanja wanataka kutumia mwanya wa njia ya MKATO kuwaingiza wawatakao madarakani kwa faida ya mfanyabiashara MMOJA TU.

Serikali haiwezi KUINGILIA MASUALA YA SOKA na hakuna kokote inaonyesha TFF imekosa au kuyumba.

Acheni kuwatisha viongozi wa TFF kwa kuisingizia serikali kwa manufaa YENU. Mlio na nafasi serikali lazima mjue ni dhamana, msizitumie VIBAYA kwa kuwasingizia viongozi wa kubwa kwa faida zenu binafsi. Maslahi ya nchi YATANGULIE.

Msiigombanishe Serikali na FIFA kwa kuwasingizia VIONGOZI WA JUU wa Serikali.

Waacheni TFF wafanye kazi ya kuendeleza mpira.

Ikumbukwe kwamba Juni 14 2025, Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa TFF, wakili Kiomoni Kibamba alitangaza rasmi kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 16 2025, jiji Tanga.

Tayari wagombea wamechukua fomu kwa nafasi mbalimbali ambapo nafasi zinazogombaniwa ni Rais 1, wajumbe wa kamati ya utendaji nafasi 6. Mwisho wa kuchukua fomu ilikuwa ni Juni 20 2025 zilianza kuchukuliwa Juni 16 2025.

Juni 21-23 kikao cha mchujo wa awali,  Juni 24-25 kubandika orodha ya wagombea waliopitishwa awali, Juni 26-28 muda wa kupokea na kuweka pingamizi, Juni 28-30 kusikiliza pingamizi, Julai Mosi-03 kufanya usaili kwa kugombea, Julai 4-5 kubandika kwenye matangazo matokeo ya awali ya ya usaili, Julai 6-8 Sekretarieti kuwasilisha masuala ya kimaadili ambacho mchakato kwa sasa bado unaendelea na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Tanga.