NYOTA wa Simba SC, Steven Mukwala amefikisha jumla ya mabao 13 ndani ya ligi. Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Juni 22 alipachika bao moja.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar. Bao hilo alipachika dakika ya 17 akiwa ndani ya 18. Mukwala alituma pasi ya David Kameta ambaye alipokea pasi elekezi kutoka kwa kiungo mshambuliaji Jean Ahoua.
Kameta kwenye mchezo wa funga kazi Uwanja wa KMC Complex alikomba dakika 90. Alishuhudia beki mwingine anayecheza upande wake Shomari Kapombe naye akiingia kwenye mchezo huo. Kapombe alipoingia Duchu alikuwa mchezaji huru akicheza kila eneo na alikuwa akipewa maelekezo mara nyingi na Kapombe.
Mukwala anafikisha mabao 13 kwenye ligi akiwa saw ana Leonel Ateba wa Simba SC huku akiwa saw ana Clement Mzize na Prince Dube wa Yanga SC na Jonathan Sowah wa Singida Black Stars ambaye alifunga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
Kinara kwenye chati ya ufungaji wa mabao ndani ya ligi ni Jean Ahoua wa Simba SC ambaye amefunga jumla ya mabao 16. Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar hakukomba dakika 90 wala hakufunga.
Mukwala alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo dhidi ya Kagera Sugar baada ya dakika 90 ikiwa ni tuzo ya mwisho kwa Simba SC kwenye ligi wakiwa kwenye mchezo wa nyumbani ndani ya msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.