MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga SC ambacho kimefunga raundi ya 30 kwa ubao kusoma Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji, Juni 22 kuna hatihati kuukosa mchezo wa Kariakoo Dabi, Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.
Ni Prince Dube ambaye hakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa raundi ya 28 dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Juni 18 2025, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kwenye mchezo huo Dube alikomba dakika 22 nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama ambaye alifunga bao moja dakika ya 35 akitumia pasi ya Clement Mzize wakati ubao ukisoma Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC.
Ndani ya ligi namba nne kwa ubora, Dube kafunga mabao 13 akitengeneza pasi 8 za mabao ikiwa ni msimu wake wa kwanza kuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Dube ni mchezaji wa kwanza kufunga hat trick msimu wa 2024/25 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Yanga SC imefunga jumla ya mabao 81 baada ya mechi 29 ikiwa ni timu namba moja kufunga mabao mengi. Dube kahusika kwenye mabao 21.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.