KAGERA SUGAR YASHUKA DARAJA RASMI, SIMBA YAPIGILIA MSUMARI WA MWISHO

Ni rasmi sasa! Kagera Sugar imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba SC kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kagera Sugar, moja ya timu zenye historia ya muda mrefu katika ligi hiyo, sasa inajiandaa kwa maisha ya Championship msimu ujao.