YANGA SC YAPIGA MTU 9 KWENYE LIGI

YANGA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kwa msimu wa 2024/25 imempiga jumla ya mabao 9-0 mpinzani wake Tanzania Prisons kwenye mechi mbili za ligi katika msako wa pointi tatu.

Yanga SC imekomba pointi sita mazima ikijikita kileleni ndani ya ligi ambayo inakaribia kugota mwisho Juni 25 2025.

Juni 18 2025 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ulisoma Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC.

 Desemba 22 2024 walipokutana  Uwanja wa KMC Complex ulisoma Yanga 4-0 Tanzania Prisons. Mzunguko wa pili Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC Juni 18 2025. Tanzania Prisons wameshindwa kufurukuta mbele ya Yanga ndani ya dakika 180.

Jumla Tanzania Prisons kwenye mechi mbili imefungwa mabao 9 huku safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ikikwama kufunga mbele ya Yanga SC nje ndani.

Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 76 baada ya mechi 28 mchezo ujao ni dhidi ya Dodoma Jiji ambao utakuwa ni raundi ya 30.

Kituo kinachofuata kwa Yanga SC baada ya Dodoma Jiji ni Kariakoo Dabi, Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa kwa watani hawa wa jadi kukutana mzunguko wa pili.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.