FOUNTAIN GATE VS AZAM FC PATACHIMBIKA

Mchezo wa Fountain Gate vs Azam FC, Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa Juni 22 2025 patachimbika uwanjani kwa wababe hao kuvuja jasho kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Fountain Gate hesabu kubwa ni kujinasua kutoka mstari wa kucheza play off huku Azam FC hesabu kubwa ikiwa ni kumaliza ndani ya tatu bora ikiwa na pointi nyingi.

Tayari Azam FC ina uhakika kugotea nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 60 na Singida Black Stars ni nafasi ya nne ikiwa na pointi 56 hata ikishinda mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons haitaishusha Azam FC.

Kete ya maamuzi kwa Fountain Gate ambayo haijawa na mwendo mzuri mzunguko wa pili. Pointi zake ni 29 kibindoni baada ya mechi 29 wastani wa kukusanya pointi moja kwenye kila mchezo. Inakutana na Azam FC iliyotoka kuvuna pointi tatu kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Tabora United, Uwanja wa Azam Complex.

Fountain Gate ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 29, ikiwa itashinda itafikia pointi 32 ambazo zipo mikononi mwa Namungo FC, hivyo dua zao ni matokeo ya Namungo FC dhidi ya KenGold kuwa wanavyoomba ili wasicheze hatua hiyo na kuwaombea Tanzania Prisons kwenye mchezo ujao dhidi ya Singida Black Stars.

Ni kikombe kizito kwa Fountain Gate ya Ofisa Issa Mbuzi kutokana na nafasi waliyopo na aina ya wapinzani ambao watakutana nao.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.