UBAO wa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ikiwa ni mchezo wa ligi mzunguko wa pili Yanga SC wamekomba pointi tatu muhimu ikiwa ugenini na kuendelea kujikita kileleni.
Ubao umesoma Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC, mabao ya Mudathir Yahya dakika ya 31, Clatous Chama dakika ya 35, Pacome dakika ya 56 na 76 huku Israel Mwenda akipachika bao moja dakika ya 60 ya mchezo.
Yanga SC wanaongoza ligi wakiwa na pointi 76 huku watani zao wa jadi Simba SC wakiwa nafasi ya pili na pointi 75 msimu wa 2024/25.
Kiungo Pacome ametupia mabao mawili akifikisha mabao 11 ndani ya ligi na pasi zake ni 9 hivyo kahusika kwenye jumla ya mabao 20 ndani ya msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.