MAKIPA WA SIMBA SC KWENYE KAZI UGENINI

SIMBA SC ikiwa imecheza mechi 27 ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora kipa Ally Salim amekaa langoni mechi mbili.

Mechi 25 langoni ni Mousa Camara ambaye ni kinara katika kukusanya hati safi akiwa nazo 17 anafuatiwa na Djigui Diarra wa Yanga SC mwenye hati safi 15.

Salim kwenye dakika 180 za ligi hakufungwa hivyo anazo hati safi mbili msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa.

Camara katika mechi 25 ambazo ni dakika 2,250 katunguliwa mabao 11 akiwa langoni katika kutimiza majukumu yake.

Makipa hao wa Simba SC leo Juni 18 2025 watakuwa na kazi kwenye kutimiza majukumu yao ndai ya Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Huenda Camara akaanza kikosi cha kwanza kuwa maumivu ambayo alipata kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali dhidi ya Singida Black Stars yamepona.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.