UBAO wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi umesoma KenGold 0-5 Simba SC ikiwa ni mchezo wa ligi mzunguko wa pili.
Ni Juni 18 2025 mchezo huo umekamilika ambapo kipindi cha kwanza Simba SC ilifunga mabao ndani ya dakika 30 na kipindi cha pili kiungo mshambuliaji Ahoua alipachika bao moja kwenye mchezo huo.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na Kibu Dennis ambaye katupia mabao mawili dakika ya 20, 25, Ellie Mpanzu amepachika bao moja dakika ya 22, Leonel Ateba dakika ya 36 alipachika bao la nne.
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC alipachika bao moja dakika ya 75 akifikisha mabao 16 ndani ya ligi.
Simba SC inafikisha pointi 75 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na vinara ni Yanga SC wenye pointi 76 tofauti yao ni pointi moja pekee ndani ya ligi msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.