Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewataka waombaji wote wa nafasi ya uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti 16 mwaka huu Jijini Tanga kuhakikisha wanakuwa na Kanuni za Uchaguzi.
Taarifa ya leo Juni 17, 2025 iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa wagombea hao wanapochukua fomu za kuwania uongozi katika uchaguzi huo wanatakiwa kuhakikisha wanapata na Kanuni hizo na kubainisha kuwa kwa wale ambao tayari wameshachukua fomu, wanatakiwa kuwasiliana na Sekretarieti ya TFF ili kupata Kanuni hizo.
TFF imesema nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo utakaoendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF ni saba. Nafasi hizo ni Rais, na wajumbe sita wa Kamati ya Utendaji.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni saa 10 kamili jioni Agosti 20 mwaka huu. Fomu zinarudishwa katika ofisi za TFF.