UONGOZI wa Singida Black Stars umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya kutwaa ubingwa mbele ya Yanga SC kwenye mchezo wa fainali CRDB Cup unaotarajiwa kuchezwa Juni 28, 2025 Uwanja wa New Amaan Complex ikiwa ni funga kazi msimu wa 2024/25.
Husssen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars ameweka wazi kuwa wanatambua kuna ugumu mbele yao lakini wapo tayari kufanya kazi kubwa kupata matokeo chanya katika mechi ambazo zipo ndani ya msimu wa 2024/25.
“Kazi kubwa ilifanyika kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba SC ambao tulishinda kwa ushindi wa mabao 3-1 ulikuwa ni mchezo mgumu na mwisho tukapata matokeo mazuri tukapata nafasi kutinga fainali.
“Tulirudi Singida nakuanza maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utakuwa Juni 18 2025 ugenini kisha tutarejea nyumbani Singida kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao tutacheza tukiwa nyumbani ambao utakuwa ni mchezo wetu wa mwisho wa ligi Juni 22 Uwanja wa Liti.
“Baada ya michezo miwili tutakuwa na mchezo wa fainali tutakuwa ugenini dhidi ya Yanga SC Uwanja wa Amaan Zanzibar ambao ni mchezo wa mwisho hivyo tunakwenda kupambana kupata ushindi katika mchezo wetu.
“Tuliwaambiwa mashabiki wetu kwamba tutafanya kazi kubwa kufanya vizuri imekuwa hivyo unaona tumekata tiketi ya kutinga hatua ya fainali na kupata tiketi kushiriki mashindano ya kimataifa. Kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga SC tunakwenda kukutana na mabingwa watetezi lakini tupo tayari kwa kuwa tunataka kuona kwamba tunapata taji la kwanza ambalo ni muhimu kwetu na tunakwenda kwa umakini kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa Juni 28.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.