SIMBA KUREJEA KAMBINI JUNI 16 KWA MAANDALIZI YA MECHI DHIDI YA KENGOLD

SIMBA SC wanatarajiwa kurejea kambini leo Juni 16 2025 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya KenGold utakaochezwa Juni 18.

Ikumbukwe kwamba Simba SC walikuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Kariakoo Dabi ambao ulitarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 na walipewa ruhusua kufanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa, Juni 14 2025.
Ngoma ilikuwa nzito baada ya mchezo huo kubadilishwa tarehe na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Juni 13 2025 na utachezwa Juni 25 2025 kukamilisha mzunguko wa pili.

Baada ya mchezo kupelekwa mbele, Simba SC walivunja kambi na wachezaji kupewa mapumziko wanatarajia kurejea kambini leo Juni 16 2025 kwa maandalizi ya mechi zijazo.