CHAMA AANDALIWA KUIKABILI TANZANIA PRISONS

Clatous Chama kiungo mshambuliaji wa Yanga SC anaandaliwa na benchi la ufundi kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao Tanzania Prisons.

Yanga SC iliyo nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi 73 inatarajiwa kukutana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 13 na pointi 30 Juni 18 Uwanja wa Sokoine.

Kwenye mazoezi ambayo yanafanyika Chama amekuwa akipewa maelekezo na benchi la ufundi ili kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa sehemu ya mchezo Mbeya.