RASMI Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) imeusogeza mbele mchezo wa Kariakoo Dabi ambao ni namba 184 kati ya Yanga SC vs Simba SC uliopangwa kuchezwa Juni 15 2025, Uwanja wa Mkapa.
Taarifa rasmi iliyotolewa Juni 13 2025 na TPLB imeeleza imeusogeza mbele mchezo huo wa watani wa jadi mpaka Juni 25 2025.
Taarifa hiyo imeeleza namba hii: “Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) imeusogeza mbele mchezo wa NBC namba 184 kati ya Yanga SC uliotarajiwa kuchezw Juni 15 2025 mpaka Juni 25 2025, bodi inawatakia maandalizi mema.”
Yanga SC Juni 13 2025 walitoa tangazo la kwanza la mechi kuelekea Juni 25 2025 na kuandika ujumbe kwamba Hii Haina Kipengele.
Ikumbukwe kwamba mchezo huo awali uliahirishwa Machi 8 2025 na kupangiwa Juni 15 2025 ambayo ni Jumapili, Simba SC walikuwa kwenye maandalizi na Juni 13 2025 walipata barua ya kibali cha kufanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa.
Juni 13 2025, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kupitia kwa Katibu Mkuu, Wilfred Kidao lilitoa taarifa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto amewasilisha barua ya kujiuzulu na Almas Kasongo CEO wa Bodi ya Ligi amesimamishwa kazi na Rais wa TFF, Wallace Karia.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.