Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inapenda kuwataarifu wadau wote wa mpira wa miguu kuwa Uchaguzi Mkuu wa TFF utafanyika tarehe 16 Agosti, 2025 katika jiji la Tanga.
Nafasi Zitakazogombewa:
Rais wa TFF – Nafasi 1
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji – Nafasi 6
Gharama za Fomu za Kugombea:
Rais: TSh 500,000
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji: TSh 200,000
Utoaji wa Fomu:
Fomu zitatolewa kuanzia Jumatatu, tarehe 16 Juni hadi 20 Juni 2025, saa 10:00 jioni.
Fomu zinapatikana katika Makao Makuu ya TFF na pia kupitia tovuti rasmi ya TFF: www.tff.or.tz
Wadau wote wenye sifa na nia ya kugombea nafasi tajwa, mnakaribishwa kuchukua fomu ndani ya muda uliopangwa.
Imetolewa na:
Kamati ya Uchaguzi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
14 Juni 2025