SIMBA YASEMA ITACHEZA MCHEZO DHIDI YA YANGA JUNI 15 KAMA ILIVYOPANGWA

Klabu ya Simba imesema itaingia uwanjani Juni 15, 2025 kwa ajili ya kushiriki mchezo namba 184 dhidi ya Yanga SC kama ilivyopangwa na Bodi ya Ligi Kuu.

Aidha, imesema mabadiliko yoyote ya kujaribu kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu, na kwamba haitashiriki mchezo wowote wa namba 184 isipokuwa ule uliopangwa kuchezwa Jumapili.