MUKWALA HESABU ZAKE NDEFU SIMBA SC

MSHAMBULIAJI wa Simba SC Steven Mukwala hesabu zake ni ndefu kwenye kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids katika mechi za ushindani.

Mukwala ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kuona timu hiyo inapata matokeo chanya kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja msimu wa 2024/25.

Mshambuliaji huyo anaingia kwenye orodha ya wakali wakucheka na nyavu Bongo akiwa katupia mabao 12 na kutoa pasi tatu za mabao akihusika kwenye mabao 15 ndani ya kikosi cha Simba SC ambacho kimefunga mabao 63.

Kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa Uwanja wa KMC, Mukwala alifunga bao pekee la ushindi lililoipa pointi tatu Simba SC kwenye mchezo huo na alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

“Kazi ni kubwa kwenye mechi ambazo tunacheza na mpango ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya inawezekana na tunashirikiana na benchi la ufundi kuona kwamba matokeo yanapatikana.”

Mchezo ujao kwa Simba SC ni Juni 15 2025 dhidi ya Yanga SC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa huku Yanga SC ambao ni wenyeji wakibainisha kwamba hawapo tayari kwa mchezo huo namba 184 mpaka matakwa yao manne yatimizwe.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.