JEMBE SPORTS YOU TUBE YAPEWA TUZO MAALUMU

SHUKRANI kubwa kwa watazamaji na wafuatiliaji wa mtandao wa Jembe Sports kwa kuwa ni watu muhimu kila wakati jambo lililopelekea tuzo maalumu kutoka kwa You Tube.

Kwenye ukurasa wa You Tube wa Jembe Sports ni watazamaji zaidi ya laki moja wapo na watu ambao wamebofya kile kitufe cha kuifuata You Tube ya Jembe Sports ni zaidi ya laki moja.

Kutokana na hilo You Tube wametoa tuzo maalumu kwa kufikisha wafuatiliaji zaidi ya laki moja hakika hii ni kubwa sana na tunajivunia wewe mtazamaji wetu wa thamani kubwa.

Juni 12 2025 Tuzo imefunguliwa rasmi kutoka kwenye boxi na sherehe fupi kuwapongeza wafanyakazi na wafuatiliaji wa Jembe Sports imefanyika.

Hii keki ni maalumu kwa wale ambao walikuwa Dar Juni 12 2025, nyie wa mbali hatujawatenga na hatujawasau sio kesi kazi yetu itakuwa ni kuwapa kile kilicho bora zaidi.

Itakumbukwa kwamba miongoni mwa wale waliofanya kazi kukupa taarifa za kimichezo ni Isaya Dede mzee wa kujikung’uta upupu kisha Ally Mzuri anaendelea na gurudumu.

Asante sana mtazamaji wetu, keki yako ni habari bora na zenye uhakika.