ZIKIWA zimesalia siku tatu kufika Juni 15 2025 siku ambayo mchezo wa Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa kati ya Yanga SC ambao ni wenyeji na Simba SC ambao watakuwa ugenini, wageni Simba SC wamegoma mchezo namba 184 ikiwa utafanyiwa mabadiliko.
Ipo wazi kwamba Yanga SC, Juni 9 2025 walitoa taarifa kuwa hawapo tayari kwa mchezo namba 184 ambao uliahirishwa Machi 8 2025 kwa kubainisha kuwa ili wacheze lazima matakwa yao manne yafanyiwe kazi.
Matakwa ya Yanga SC ni pamoja na kujiuzulu kwa CEO Bodi ya Ligi Kuu Bara, Almasi Kasongo, kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, bodi huru na kupewa zawadi ya ubingwa wa CRDB Federation Cup
Rasmi Juni 12 2025 Simba SC wamebainisha kuwa mabadiliko yoyote ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 yakitokea yatakuwa batili.
Taarifa imeeleza; ” Klabu ya Simba inauarifu umma, wanachama na wapenzi wake kuwa itaingia uwanjani siku yavJumapili, Juni 15 2025 kushiriki mchezo namba 184 kama ilivyopangwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.
Mabadiliko yoyote ya kujaribu kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu.
Kwa msingi huo, Klabu ya Simba haitashiriki mchezo wowote wa namba 184 isipokuwa ule uliopangwa kuchezwa siku ya Junapili Juni 15 2025.
Tunawaomba wanachama na wapenzi wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kuijaza Benjamini Mkapa siku hiyo muhimu ili kuiunga mkono timu yetu.
Ilieleza taarifa hiyo ya Simba SC, Juni 12 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.