AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa mchezo wa Kariakoo Dabi, Jumapili Juni 15 2025 upo palepale.
Ipo wazi kwamba wenyeji wa mchezo huo ni Yanga SC ambao wameweka wazi kwamba hawatacheza mchezo huo mpaka matakwa yao manne yatakapotimizwa na watakuwa tayari kucheza mchezo wa Kariakoo Dabi tarehe nyingine sio Juni 15 2025.
Ahmed amesema: “Ninachoweza kuwathibitishia Wanasimba ni kuwa kauli ya Simba SC ni moja tu, mechi ya Juni 15 2025 maarufu kama Kariakoo Dabi ipo palepale kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa na Bodi ya Ligi.
“Mwanasimba usiyumbishwe, usitetereke mechi namba 184 ipo palepale hivyo usisikilize wengine tusikilize viongozi wa Simba SC kuelekea katika mchezo husika tunakuambia nini.
“Tayari baada ya kurejea kutoka kwenye mchezo wetu wa FA kutoka Babati, Manyara tumeanza maandalizi kuelekea mchezo wetu ujao wa Juni 15 2025 na tumewaambia wachezaji, benchi la ufundi kwamba wao wasisikilize ngojera za nje hayo ya nje wawaachie watu wa nje, tupo sawasawa kuelekea Juni 15.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.