CHE MALONE KAZI IPO SIMBA SC

BEKI wakupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Simba SC, Che Malone kazi ipo kuelekea msimu wa 2025/26 ambapo anatajwa kuwa kwenye hesabu za kukutana na Thank You.

Beki huyo ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids hajawa kwenye mwendelezo mzuri kwenye mechi za ushindani za hivi karibuni.

Simba SC imepishana na mataji mawili makubwa ikiwa ni Kombe la Shirikisho Afrika na CRDB Federation Cup kutokana na safu ya ulinzi kukwama kuzuia na ile ya ushambuliaji kushindwa kufunga.

Katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane kwenye mechi mbili Simba SC ilifungwa mabao 3-1 na kwenye nusu fainali CRDB Federation Cup Simba SC ilifungwa mabao 3-1 dhidi ya Singida Black Stars.

Taarifa zinaeleza kuwa beki huyo amepewa masharti maalumu na benchi la ufundi linafuatilia kwa ukaribu maendeleo yake ili kubaki naye ndani ya kikosi ama kuachana naye mazima raia huyo wa Cameroon.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.